Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa 41 mbaroni wizi wa simu

Be1b785be6e1410f40e165fa8eb010eb Watuhumiwa 41 mbaroni wizi wa simu

Mon, 7 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

POLISI mkoani Morogoro kwa kushirikiana na kitengo cha makosa ya wizi kwa njia ya mtandao, imeunda kikosi kazi cha kudhibiti matukio ya wizi wa simu za mkononi na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 41 kwa kipindi cha wiki mbili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, alisema watuhumiwa hao ni kati ya 48 waliokamatwa kufuatia opereshani iliyofanyika Agosti 14 hadi 30, mwaka huu.

Alisema baadhi ya watuhumiwa walikamatwa na mafuta ya aina ya dizeli lita 1,240, pombe ya gongo lita 124, viroba 10 vya mbegu, na gari moja aina ya Peugeot lililokutwa na mtuhumiwa wa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Alisema, watu 41 wanatuhumiwa kujihusisha na wizi wa simu za mkononi 85 za aina mbalimbali, kompyuta sita zikiwa na programu za kuflash simu, na pikipiki nne zilizotumika katika matukio ya uporaji wa simu.

Kwa mujibu wa Mutafungwa, watuhumiwa 12 wanadaiwa kuwai mafundi wazoefu kubadilisha namba za IMEI na kuflash simu za wizi wakiwemo Amos Mapunda mkazi wa Mtaa wa Kididimo Manispaa ya Morogoro na Paul Dotto, mkazi wa Ngoto Manispaa ya Morogoro.

Watuhumiwa wengine wa uporaji simu kwa kutumia pikipikikuwa ni Abbas Hassan mkazi wa Msamvu, Emmanuel Madega, Mohammed Dundo, Ally Chombo na Kelven Lotiloti.

Wengine waliokamatwa wakidaiwa kuwa wapokeaji na wauzaji wa simu ni Mengi Seleman, Zaid Hamis na watuhumiwa wa wizi wa simu katika kumbi starehe ni Jailos Mankis , Joshua Cosmus na Omary Suleymani.

Kamanda Mutafungwa alitaja aina ya simu za mkononi 85 zilizokamatwa kuwa ni Iphone, Sumsung, Infinix na Techno, wakati kompyuta sita ni za aina ya laptop nne, desktop mbili zenye programu za kuflash simu na kubadilisha IMEI namba.

Aidha, alitaja pikipiki nne zilizokamatwa na wezi hao kuwa ni zenye namba MC 832 CHP aina ya Haojue, MC 279 CJK aina Haojue, T 162 CJV aina ya SanLg na moja aina ya Houje isiyo na namba za usajili.

Alitaja maeneo ambayo wahalifu hao walikuwa wakifanya matukio yao ya uporaji ni kuwa ni klabu za usiku za maeneo ya Msamvu, Chamwino, Nane Nane, Kigurunyembe, Mafiga na maeneo yenye mkusanyiko wa watu hasa sehemu za minada , masoko na vyuo vikuu.

Alisema misako hiyo itakuwa endelevu na Polisi imejipanga kudhibiti na kukamata watuhumiwa wote wanaojihusisha na matukio hayo.

Chanzo: habarileo.co.tz