Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa 24 mauaji ya polisi Ngorongoro waachiwa huru

Hukumu Pc Data Watuhumiwa 24 mauaji ya polisi Ngorongoro waachiwa huru

Tue, 22 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru washtakiwa wote 24 wa kesi ya mauaji ya Askari Koplo Ganus Mwita, yaliyotokea Juni 10 mwaka huu katika Kijiji cha Orlolosokwani Tarafa ya Loliondo Wilayani Ngorongoro – Arisha.

Washtakiwa hao wakiwemo wananchi na viongozi wa chama na serikali katika Tarafa ya Loliondo, wameachiwa huru baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Shauri hilo limeondolewa chini ya kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya mwenendo sa makosa ya jinai.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Mahakamani hapo June 16 mwaka huu mbele ya Hakimu Herieth Mhenga wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, ambapo ilikuwa na jumla ya washtakiwa 27 na baadaye watatu kuaachiwa na hivyo kufanya idadi ya washtakiwa kusalia 24.

Katika kesi hiyo, upande wa Jamhuri ulikuwa ukiwakilishwa na wakili Upendo Shemkole, huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na mawakili Jebra Kambole, Yonas Masiay,Mhyela Ally na Denis Mosses.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live