Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watuhumiwa 13 mbaroni kwa kuchoma moto basi

Basi Motooo (1).jpeg Watuhumiwa 13 mbaroni kwa kuchoma moto basi

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limesema mpaka sasa wamefanikiwa kuwakamata Jumla ya Watuhumiwa Kumi na Tatu (13) kuhusiana na Tukio la Kuchoma gari namba T.668 BCD Scania Mali ya Kampuni ya Sai Baba, katika Kata ya Msambiazi, Tarafa ya Korogwe, wilaya ya Korogwe.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Alimachius Mchunguzi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi yake Jijini Tanga ambapo amesema Mara baaa ya Upelelezi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani

Amesema katika Tukio hilo, Basi la SAI BABA likiendeshwa na Seasa Frank Chuwa (48) Mkazi wa Dar es Salaam likitokea katika Mkoa huo kuelekea mkoa wa Arusha liligongana na Pikipiki namba MC 819 EAF aina ya Hajoue iliyokuwa ikiendeshwa na Awadh Issa Juma (20) Mkazi wa Mtonga Korogwe akitokea Msambiazi kuelekea Korogwe na kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Pikipiki na Uharibifu wa Gari.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa wito kwa Baadhi ya Wananchi ambao bado wanaendelea kujihusisha na vitendo vya kihalifu kuacha kwani wakiendelea Jeshi halitosita kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live