Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu watatu wafikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji yaliyotokea miaka 20 iliyopita

RUNGU Walisomewa umri wao wakati wakifanya uhalifu wao mwaka 2002

Tue, 19 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watuhumiwa hao ni wakazi wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Masasi kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke aliyetambulika kwa majina ya Nora Hamisi.

Nora aliyekuwa Mkazi wa Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, aliuawa na mwili wake kutupwa katika Mtaa wa Machinjioni katika Kata ya Mkuti.

Watuhumniwa hao walifikishwa kortini mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu wa Wilaya ya Masasi, Batista Kashusha na kusomewa mashtaka ya mauaji wanayodaiwa kuyafanya miaka 20 iliyopita.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi Insepta Jovina alidai kuwa watuhumiwa hao wanakabiliwa na kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2002 mbele ya Mahakama hiyo.

Aliwataja watuhumiwa hao na umri wao ulivyokuwa wakati wa tukio ni; Rajabu Songo (34), kazi wa mtaa wa Machinjioni, Kata ya Mkuti Wilayani Masasi, Stanley Mtweve (32), Mkazi wa Mtaa wa Makaburini Kata ya Mkuti Wilayani Masasi na Yusuph Pahala (30), mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Mkomaindo wilayani Masasi.

Inspekta Jovina alidai kuwa watuhumiwa hao walimuua Nora kisha kuuchukua mwili wake na kuutupa katika Mtaa wa Machinjioni kisha kutoweka.

Alidai waliutupa mwili eneo hilo kwa lengo la kupoteza ushahidi, lakini baada ya uchunguzi wa Jeshi la Polisi walikamatwa. Watuhumiwa hawakutakiwa kuzungumza lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kwa mujibu wa sheria, Mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ni Mahakama Kuu.

Wote walirejeshwa mahabusu na kesi hiyo itatajwa tena Aprili 24, 2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live