Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu wanne katika watu 100 wanatumia dawa za kulevya

Dawa Za Kulevya Watu wanne katika watu 100 wanatumia dawa za kulevya

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Joseph Mhagama imeitaka serikali kuunda divisheni maalumu itakayokuwa inashughulikia mashauri ya dawa za kulevya ili kuwawezesha watoa maamuzi kubobea kwenye eneo hilo,

Mhagama amesema yapo mashauri 1158 ya dawa za kulevya mahakamani na hadi sasa ni mashauri 68 pekee yamefanyiwa kazi.

Amesema matumizi ya dawa za kulevya ni janga kubwa kutokana na takwimu za kati ya mwaka 2017 hadi 2020 ambapo matumizi ya dawa za kulevya duniani yameongezeka mara nne katika kipindi hicho.

Idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya duniani kwa kipindi hicho pia imefikia watu milioni 200 sawa na asilimia nne ya watu wote duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live