Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu wanane akiwemo kigogo wa Serikali wafikishwa kortini

74986 Kizimbanipic

Mon, 9 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watu wanane akiwemo Mkemia Mwandamizi wa Serikali ya Tanzania, Everlight Matinga wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka saba.

Miongoni mwa mashtaka hayo ni la kuingiza kemikali bila ya kuwa na usajili wa bodi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ya Tanzania.

Pamoja na Matinga wengine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Teckno Net Scientific, Benedi Assey, Ofisa Utawala, Wenceslaus Assey, Meneja Masoko, Wifrida Assey, Ofisa Masoko na Manunuzi Salvatory Assey, Mtunza Stoo, Emanuel Assey, Samwel Mahalika na Matilda Temba.

Akisoma hati ya mashtaka leo Jumatatu Septemba 9, 2019 Wakili wa Serikali, Ashura Mzava mbele ya Hakimu Mkazi Vick Mwaikambo amedai kati ya Mei Mosi, 2016 na Aprili 30, 2017 mshtakiwa wa kwanza hadi wa saba walijihusisha na biashara ya kemikali yenye uzito wa lita 526.50 na kilogramu 874.50 bila ya kibali kutoka bodi ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Katika shtaka la pili, katika tarehe hiyo maeneo ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam mshtakiwa wa kwanza hadi wa saba wakijua ni takwa la kisheria ya kuwa na kibali kinachotolewa na bodi ya Maabara ya Mkemia Mkuu mlikutwa mnajihusisha na kemikali yenye uzito wa lita 526.50 na kilogramu 874.50

Shtaka la tatu, tarehe hiyohiyo na maeneo hayo mshtakiwa wa kwanza hadi wa sita huku mkijua takwa la kisheria mlikutwa mmehifadhi kemikali mbalimbali ikiwemo Laclophenol, Aceton, Acel Acid Glacial na Tricloethylene zenye uzito wa Lita 526.50 na kilogramu 874.50.

Pia Soma

Advertisement
Mzava alidai katika shtaka la nne kati ya Mei Mosi, 2016 na Mei 28, 2016 katika maeneo ambayo hayajulikani jijini Dar es Salaam washtakiwa hao pamoja na Mkemia wa Serikali mwandamizi mlitenda kosa ovu la kula njama kwa barua kutoka kwa msajili wa viwanda na watumiaji wa kemikali huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa walikana mashtaka hayo na upande wa Jamhuri walidai upelelezi haujakamilika huku Hakimu Mkazi Mwaikambo alisema dhamana kwa washtakiwa hao ipo wazi hivyo wanatakiwa wadhamini wawili wanaofanya kazi serikalini au binafsi na wawe na kitambulisho cha Taifa (Nida) na barua za utambulisho ambao watakaosaini bondi ya Sh10 milioni.

Hata hivyo, washtakiwa Wenceslaus, Wilfrida na Matinga walifanikiwa kupata dhamana na Benedict, Salvatory, Emanuel, Mahalila na Temba walishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo wamerudishwa mahabusu.

Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 23, 2019 itakapokuja tena.

Chanzo: mwananchi.co.tz