Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu saba mbaroni kwa kukutwa na baruti na vipande vya chuma

Mbaroniiiiiiiii Watu saba mbaroni kwa kukutwa na baruti na vipande vya chuma

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

eshi la Polisi Mkoani Singida kwa Kushirikiana na Maafisa wa Wanyamapori Wilayani Manyoni limewakamata watu saba kwa Tuhuma za kukutwa na Nyara za Serikali Pamoja na Silaha aina ya Gobore katika Msako ambao umefanyika Mapema Mwezi huu.

Akizungumza na Wanahabari Mkoani Singida Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida ACP Stella Mutabihirwa Amesema Katika Msako Huo watuhumiwa Walikamatwa wakiwa na Vipande 95 vya Chuma Pamoja na Chupa Mbili za Baruti kinyume cha Sheria ya Umiliki wa Silaha.

Aidha Amesema Jeshi hilo kwa Kushirikiana na Maafisa wa Idara ya Kupambana na Ujangili wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa Wanne wakiwa na nyara za serikali ambayo ni Kipamde cha pembe ya Mnyama faru chenye uzito wa kg 2.5.

Watuhumiwa waliokamatwa katika Tukio hilo Batholomeo Saimoni (62) Mkazi wa Heka Manyoni ,Masanja Mlingwa (45) Mkazi wa Heka Manyoni,Nichoden Ebiud (37) Mkazi Chikola Manyoni Pamoja na Emanuel Jack (45) Mkazi wa Meatu Mkoani Simiyu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live