Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 60 wakamatwa kwa kutengeneza gongo

Kamandaaa 660x400 Watu 60 wakamatwa kwa kutengeneza gongo

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Watu 60 wakazi wa Wilaya ya Rombo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanajaro kwa tuhuma za utengenezaji wa pombe haramu ya gongo na usafirishaji wa madawa ya kulevya aina ya bangi na mirungi.

Mkuu wa operesheni maalumu za Jeshi la Polisi Tanzania Kamishna msaidizi mwandamizi Mihayo Msikhela amesema watu hao wamekamatwa na lita 500 za pombe haramu ya gongo na zaidi misokoto 2300 ya bangi.

“Tumefanikiwa kukamata watuhumiwa takribani 60 vielezo vilivyopatikana ni gongo ambayo ni lita 549.2 , mitambo ya kutengeneza gongo ambayo ni 18, mapipa matupu 112, pikipiki 4, madumu tupu 38  ya lita 20 yenye rangi ya njano, ndoo mbili tupu za lita 20 , mirungi kilo 68.8, misokoto ya bangi 2340, mazao ya misitu ambayo ni mbao 497” Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mihayo

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa kilimanjaro Ronald Makona akazungumzia zoezi hilo ambalo amesema ni endelevu kwa wilaya zote za mkoa wa kilimanjaro na tiyari wana majina ya watu amabo wanaendelea kuwaorodhesha kwenye orodha yao na wataendelea kuwasaka mpaka pale watakapopatikana.

MAAFISA TBS WALIOTAKA RUSHWA MILIONI 100 WASIMAMISHWA KAZI NA KUKAMATWA NA TAKUKURU

Chanzo: millardayo.com