Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 567 mbaroni kwa uhalifu Geita

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Geita, Safia Jongo.jpeg Watu 567 mbaroni kwa uhalifu Geita

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoani Geita limewakamata watu 567 wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya mauaji, ubakaji, kukutwa na mali za wizi pamoja na dawa za kulevya aina ya bangi.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Saphia Jongo amesema watu hao wamekamatwa kwenye operesheni inayoendelea. “Operesheni hii ilianza Aprili mwaka huu, ni mwendelezo.”

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 21, 2024 Kamanda Jongo amesema mbali na kukamatwa kwa watu hao pia wamekamata bangi kete 43 na gramu 520 pamoja na pombe ya moshi (gongo) lita 416.

Mali nyingine ni mashine ya kusagia mawe, pikipiki nane vitenge majora 15, televisheni nane, magodoro matano, kompyuta nne, mafuta ya dizel lita 65 na cherehani mbili.

Kamanda Jongo amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kuliamini ili kutokomeza uhalifu kwenye mkoa huo.

Wakizungumza hali ya usalama mkoani humo baadhi ya wananchi wameiambia Mwananchi Digital kuwa jeshi hilo limejitahidi kupambana na uhalifu wa nyumba kwa nyumba uliokuwa ukifanywa nyakati za usiku, na sasa watu wanalala kwa mani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live