Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 5 washikiliwa na Polisi tuhuma wizi mafuta SGR

Wizi Pic Mafutaaa Mafutaa Watu 5 washikiliwa na Polisi tuhuma wizi mafuta SGR

Mon, 20 Mar 2023 Chanzo: mwanachidigital

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata watuhumiwa kumi (10) wa makosa mbalimbali ikiwemo wizi wa mafuta lita 302 aina ya dieseli katika mradi wa SGR.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Leonard Nyandahu amesema jeshi hilo kwa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Februari 28 hadi Machi 20, Mwaka huu 2023 limefanya misako na doria katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga na kuwakamata watuhumiwa hao.

Nyandahu ameeleza kuwa jeshi hilo limefanikiwa kukamata jumla ya lita 302 za mafuta aina ya dieseli katika maeneo tofauti ya Mradi wa Reli ya Mwendokasi SGR na kukamata watu watano (5) wanaotuhumiwa kwa wizi wa mafuta hayo na kwamba tayari wamefikishwa mahabusu kwa ajili ya hatua zaidi za kesheria ikiwemo kufikishwa mahakamani. Also Read

Mchungaji afunga kanisa kisa Sh100 milioni za 'kubeti' Kitaifa Just now Mchungaji afunga kanisa kisa Sh100 milioni za 'kubeti' Kitaifa Just now

Kaimu kamanda huyo amesema jeshi hilo pia limekamata watuhumiwa wengine watano (5) wa makosa mbalimbali, na kukamata madawa ya kulevya aina ya Bangi kilo 22, Cementi mifuko 3, pamoja na Magodoro mawili (2).

Aidha vitu vingine vilivyokamatwa ni pikipiki 4 ambazo zilikuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya uharifu, printer moja, kompyuta moja, runinga mbili, mbolea kilo 30 pamoja na betri kumi (10) za magari ambazo ziliibwa kwa kipindi na maeneo tofauti.

Nyandahu ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ikiwemo kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea kuwasihi wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kutokomeza uhalifu na pia jeshi linaahidi kuendelea kuzifanyia kazi taarifa mbalimbali za kihalifu zinazotolewa na wananchi kwa usiri mkubwa,”amesema Nyandahu.

Chanzo: mwanachidigital