Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 4,155 wachunguzwa matukio ya rushwa

55aa04157a28a90b7808c4f196e3ebd6.jpeg Watu 4,155 wachunguzwa matukio ya rushwa

Tue, 15 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATU 4,155 wamefanyiwa uchunguzi wa vitendo vya rushwa kuanzia mwaka 2018.

Katibu Mkuu wa Taasisi ya Uchunguzi wa Rushwa Rwanda (RIB), Kanali Jeannot Ruhunga alisema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Vitendo vya Rushwa nchini iliyoadhimishwa Desemba 9 mwaka huu.

Alisema mwaka 2018 ofisi yake ilifanya uchunguzi kwa watu 1,131 waliohusika katika matukio 732 ya rushwa na mwaka uliofuatia walichunguza watu 1,29 waliohusika katika matukio 1,088 na mpaka Novemba mwaka huu watu 1,29 waliohusika kwenye matukio 963 walihojiwa.

“Kumekuwa na watu wengi wanaotoa taarifa za vitendo vya rushwa lakini hata sisi tumeendelea kufuatilia vitendo hivyo ikiwamo matumizi mabaya ya fedha za umma. Kwa mfano kwa takwimu za hapo juu watuhumiwa 1,279 wamehusiaka katika uhalifu wa matumizi mabaya ya fedha za umma,” alisema.

Waziri katika Ofisi ya Rais, Judith Uwizeye alisema katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo na Biashara kuwa Afrika inapoteza dola za Marekani bilioni 888 kutokana na matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Uwazi Rwanda, Marie Immaculée Ingabire alisema inatakiwa suala la rushwa wkuangalia kwa wanaotoa na wanaopokea kwani kuna maeneo watu wamekuwa wakitoa rushwa bila kuchukuliwa hatua.

Julai mwaka huu Waziri wa Sheria, Johnston Busingye alisema serikali inatarajia kupata faranga bilioni 11 kutokana na kesi ambazo ilishinda katika matukio ya ufisadi wa fedha za umma.

Chanzo: habarileo.co.tz