Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 3 wa Familia Moja Akiwemo Mtoto Wauawa Wakilinda Mazao

Mauaji 2?fit=584%2C368&ssl=1 Watu 3 wa Familia Moja Akiwemo Mtoto Wauawa Wakilinda Mazao

Thu, 20 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

WATU watatu wa familia moja akiwemo mtoto mchanga wa miezi sita, wameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za miili yao wakiwa wamelala kwenye kibanda shambani wakilinda mazao yao.

Akizungumza leo Mei 19, 2021 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema tukio hilo limetokea Mei 18, 2021 majira ya saa mbili usiku, katika Kijiji cha Kazilamihunda, wilayani Kakonko mkoani hapa.

Kamanda amesema wakiwa shambani wamelala watu wasiofahamika waliwavamia na kuwaua ambapo, baba wa familia Masabile Kamana (58) alipata majeraha shingoni, ubavu wa kushoto, kisigino cha mguu wa kushoto na kukatwa kiganja cha mkono wa kushoto.

Amesema mkwe, Dobora Masabila, raia kutoka Burundi, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (36-42), alipata jeraha kwenye kisogo na kupasuka fuvu na jeraha katika mkono wa kulia.

“Katika tukio hilo mtoto wa miezi sita amejeruhiwa kwenye utosi na kusababisha kifo chake, huku mtoto mmoja wa familia hiyo, Janet Masabile (5), aliachwa amelala bila kujeruhiwa popote,” amesema Kamanda Manyama.

Amesema jeshi hilo linaendelea kuwasaka waliofanya mauaji hayo ili kuwachukulia hatua za kisheria na akawataka wananchi wa mkoa huo kuacha mara moja vitendo vya kujichulia sheria mkononi.

Chanzo: globalpublishers.co.tz