Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 28 mbaroni wakidaiwa kuwajeruhi polisi

49929 WANANCHI+PIC

Tue, 2 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Polisi mkoani Geita  inawashilikia wananchi 28 wa kijiji cha Nyijundu kata ya Nyang'hwale wakidaiwa kuwashambulia na kuwajeruhi  polisi watatu waliokuwa wakizuia mtuhumiwa wa ujambazi kuuawa.

Kutokana na zuio la askari wananchi wakiwa na silaha za jadi waliwavamia na kuanza kuwapiga kwa silaha za jadi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Aprili mosi 2019 kamanda wa polisi mkoani Geita, Mponjoli  Mwabulambo amethibitisha askari wake kujeruhiwa na kuwataja waliojeruhiwa kuwa ni Omari ambaye ni mkaguzi wa Polisi tarafa ya Nyangwale.

Mwingine ni askari H16 D/C Yusuph aliyejeruhiwa mguu wa kulia na H4311 D/C Joseph aliyelazwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.

Akielezea tukio hilo, Mponjoli amesema Jumamosi Machi 30, 2019 kundi la majambazi wakiwa na silaha za jadi walivamia nyumba za wakazi wawili kijiji cha Nyijundu na kumuua mkazi mmoja na kujeruhi wengine watatu kisha kupora fedha.

Amesema kufuatia hali hiyo, wananchi walipiga yowe na kuanza msako kwa kushirikiana na polisi na walipomkamata mmoja waliyedhani ni mtuhumiwa na kumhoji kisha kukiri walitaka kumuua na walipozuiwa na polisi wakawageuzia kibao.



Chanzo: mwananchi.co.tz