Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 21 mbaroni kwa wizi wa kutumia silaha za jadi

PANGA Ed Watu 21 mbaroni kwa wizi wa kutumia silaha za jadi

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoa wa mjini magharibi linawashikilia watuhumiwa 21 kwa makosa ya wizi uporaji na unyan'ganyi wa kutumia silaha za jadi

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi SACP Richard Tadei Mchomvu huko ofisini kwake madema wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusiana kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Amesema vijana hao wanajihusisha na matukio ya kihalifu ikiwemo wizi, uporaji na unyanganyi kwa kutumia silaha za jadi (mapanga) katika maeneo ya Kinuni, Nyarugusu, Mtoni, Mwera, Kwarara, Fuoni, Kwerekwe, Malindi, Bububu na Darajabovu, ambapo huwapora na kuwaibia vitu vyao hasa wakati wa usiku.

Kamanda Mchomvu amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kuwafichua wahalifu hao ili wachukuliwe hatua kali za kisheria pamoja na kufikishwa Mahakamani.

Sambamba na hayo Kamanda Mchomvu ametoa wito kwa wazazi na walezi kufuatilia tabia na mienendo ya watoto wao kwani vijana wengi wanajiingiza katika uhalifu kwa kukosa malezi bora ya wazazi na kuamua kujiingiza kwenye uhalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live