Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ulanga imewakamata watu wawili Erick Samwel na Experius Kwilinga kwa tuhuma za kutengeneza Madini feki aina ya Vito na kuyauza kwa wafanyabishara .
Mwenyekiti kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ulanga ambaye pia ni mkuu wa Wilaya hiy, Ngollo Malenya amesema wafanyabishara hao wamekamatwa baada ya baadhi ya wafanyabishara kulalamika kutapeliwa kuuziwa Madini feki.
Dc Malenya amesema wafanyabishara hao wamekua wakichukua mawe kisha kuyapaka wino wa peni na kukausha juani mawe hayo na baada muda huyauza katika soko la Madini wilayani humo.
Dc Malenya ametoa wito kwa wafanyabishara wakiotaotapeliwa kutoa taarifa katika ofis yake huku akito onyo kwa watu wengine kiacha kufanya michezo hiyo
Watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapo kamilika watafikoshwa katika mamlaka husika kujibu tuhuma zinazowakabili.