Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 18 wakamatwa na samaki wachanga kilo 125

10121 Samaki+pic TanzaniaWeb

Sat, 4 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu 18 wakituhumiwa kufanya makosa mbalimbali ya kihalifu likiwamo kupatikana na samaki wachanga kilo 125 wilayani Sengerema.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi kwa vyombo vya habari Agosti 4 mwaka huu imesema kuwa watu hao pia walikamatwa wakiwa na nyavu haramu 50 za kuvulia samaki aina ya timba pamoja na madawa ya kulevya aina ya bangi kilo mbili.

Kamanda Msangi amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika operesheni maalum iliyofanyika kwa siku mbili kuanzia Agosti 2 hadi 3 katika maeneo mbalimbali ndani ya Ziwa Victoria iliyoshirikisha polisi wanamaji, askari wa wilaya ya Sengerema na kuongozwa na opereshenu Ofisa wa mkoa wa Mwanza, Audax Majaliwa na Mkuu wa polisi wilayani ya Sengerema, Mairi Wassaga.

“Watuhumiwa hao pia walipatikana na pombe  aina ya gongo lita 265, pikipiki moja inayodaiwa ni ya wizi pamoja na nyavu haramu 600 za kuvulia dagaa kitendo ambacho ni kosa la jinai,” amesema Msangi.

Kamanda Msangi amesema polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kuwa katika baadhi ya maeneo ya vijijini pembezoni mwa Ziwa Victoria na katika visiwa vilivyopo wilayani sengerema wapo watu wanaojihusisha na biashara haramu ya pombe na uuzwaji wa madawa ya kulevya.

Lakini pia raia hao walisema maeneo hayo kuna matukio ya wizi wa vitu mbalimbali, uvuvi wa samaki wachanga na vitendo vingine vya kihalifu.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz