Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 17 wakamatwa wakitaka kuwafanyia mtihani wahitimu Chuo Kikuu Huria

Prof. Elifas Bisanda.png Watu 17 wakamatwa wakitaka kuwafanyia mtihani wahitimu Chuo Kikuu Huria

Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 17 wamekamatwa kwa tuhuma za kutaka kuwafanyia Mitihani Wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) katika Vituo vya Ilala (Watuhumiwa 13) na Kinondoni (Watuhumiwa 4)

Makamu Mkuu wa OUT, Prof. Elifas Bisanda ameliomba Jeshi la Polisi kuwafikisha Mahakamani haraka Watuhumiwa ambao asilimia kubwa ni Watu wa Nje na hawana uhusiano na Chuo, akidai walitumia Vitambulisho vya wale waliotaka kufanyiwa Mitihani na wengine walighushi Vitambulisho jambo ambalo ni kosa la Jinai

Ameongeza “Hatujui wamelipwa kiasi gani, matukio yalianza kuripotiwa Juni 18, 2024, tuliwakamata kwa msaada wa Wasimamizi wetu na Maafisa wa Usalama wa Taifa. Tupo tayari kutoa ushirikiano kwa Polisi, vielelezo vyote tunavyo. Sitaridhika kusikia wanaendelea na upelelezi wakati ushahidi wote upo na nitaifikisha taarifa hii kwa IGP na Ofisi ya Rais.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live