Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 15 Mbaroni kwa Kukutwa Wakiuza Jezi Feki

Jezi Feki (1) Watu 15 Mbaroni kwa Kukutwa Wakiuza Jezi Feki

Thu, 16 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa 15 kwa tuhuma za kuuza jezi feki kutoka katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Tabora na Tunduma ambapo jumla ya Jezi 279, Urembo (ribons) 300 na Kofia sita zimekamatwa.

Katika taarifa ya jeshi polisi wameeleza kuwa kesi zimefunguliwa dhidi yao na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha katika uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo umebaini uwepo wa wafanyabiashara waliofanya mawasiliano na viwanda vya ndani na nje ambavyo jezi halali hutengenezwa wakitoa oda ya kutengenezewa jezi feki.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa watu wanaofanya vitendo hivyo kuacha kwani watachukuliwa hatua endapo wataendelea kufanya uhalifu huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live