Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 148 mbaroni kwa uhalifu Simiyu

Simiyu 0010 Watu 148 mbaroni kwa uhalifu Simiyu

Sun, 19 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linawashikilia watu 148 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo wizi wa mali, kukutwa na bangi, mirungi, pamoja na nyara za serikali zikiwemo pembe za ndovu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, (ACP) Edith Swebe amesema watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika operesheni ya kupambana na uhalifu pamoja na madawa ya kulevya iliyofanyika mwezi Aprili.

Amesema kuwa baadhi ya watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika, huku wengine wakiwa bado hawajafikishwa kwenye chombo hicho cha kutoa haki kutokana na upelelezi kutokamilika.

Kati yao, watuhumiwa saba wamekamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya mirungi na bangi, watuhumiwa sita kwa nyakati tofauti wamekamatwa wakiwa jumla ya mabunda 1160 ya mirungi yakisafirishwa kutoka wilayani Tarime mkoani Mara kwenda jijini Mwanza.

“Jumla ya magari manne yamekamatwa kuhusika na tuhuma za usafirishaji wa madawa ya kulevya hayo ambayo ni Toyota Passo Sette yenye namba za usajiri T.961 EAM, Toyota Harrier yenye Namba za usajiri T.997 DMK, Toyota Noah Vox yenye Namba za Usajiri T.307 AMG pamoja na Toyota Probox yenye namba za usajiri T 489 EFR,” Amesema Swebe.

Ameongeza kuwa katika Kijiji cha Bushashi kilichopo Wilaya ya Maswa, mtuhumiwa mmoja amekamatwa akiwa na magunia mawili yakiwa na bangi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live