Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 11 washikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kudurufu CD za filamu

Cd Mtambo Pic Data Watu 11 washikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kudurufu CD za filamu

Tue, 25 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (Cosota) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamefanya ukaguzi wa kushtukiza katika baadhi ya maduka yanayouza Filamu mbalimbali katika eneo la Kariakoo na kufanikiwa kuwakamata watu 11, ambao wanadaiwa kudurufu filamu za nje, kinyume cha sheria.

Operasheni hiyo imefanyika mwishoni mwa wiki, katika maeneo matatu yaliyopo katika mtaa wa Aggrey na Muheza eneo la Kariakoo.

Mbali na kuwakamata watu hao, pia wamekamata mashine zilizokuwa zinatumika kudurufu CD za filamu za nje, huku CD zaidi ya 300 zikikutwa zimedurufiwa katika Ofisi za Kampuni ya Sanyiwa Production.

Ofisa Mkaguzi wa Hakimiliki Tanzania (Cosota) Paul Makula, alisema lengo la kufanya operesehni hiyo ya kushtukiza ni kukamata kazi zote zinazozalishwa kinyume na sheria ya Hakimiliki.

Makula alisema ili uzalishe kazi hizo mhusika anatakiwa awe na mkataba unaonyesha kuwa anatakiwa kuzalisha kazi hiyo.

Alisema kuwa kumekuwa na kunazalisha kazi nyingi bila kufuata utaratibu, hali inayopelekea kuua soko la kazi za sanaa nchini.

"Kumekuwa na watu wengi wakidurufu filamu mbalimbali na kuzipeleka sokoni na hivyo kufanya wale wahusika kwa kazi zao kushindwa kunufaika" alisema Makula.

Kwa upande wake, Ofisa Elimu na Uhusiano kutoka Cosota, Anitha Jonas, moja ya kazi ya taasisi hiyo ni kusimamia haki miliki zote za kazi za ubunifu mfano, kazi za sanaa, mifumo, uandishi wa vitabu pamoja na aina zote zinazohusisha masuala ya ubunifu.

"Sheria inasema mtu haruhusiwi kudurufu kazi ya mtunhata kama ni ya msanii wa Tanzania, lakini katika operesheni hii, tumeona baadhi ya watu wanaouza filamu, wakiduru CD za Filamu kinyume Cha sheria" alisema Jonas.

Miongoni mwa watu waliokutwa na CD 300 zilizodurufiwa ambazo ni filamu za nje, ni Frank Manyama ambaye alisema kuwa yeye ni msimamizi wa ofisi, hivyo anayetakiwa kuongelea suala hilo ni bosi wake.

"Mimi ni msimamizi wa ofisi ya kampuni ya  Sanyiwa Production, nina miezi sita tangu niwepo katika ofisi hii, hivyo kama mnakitu cha kuuliza muulizeni bosi wangu" alisema Manyama.

Hata hivyo katika chumba hicho kulikuwa na mashine nane za kudurufu CD (Dublicater Mashine) ambapo kila mashine inauwezo wa kudurufu CD 40 hadi 44 ndani ya dakika nane hadi 10 na hapo inategemea na aina ya filamu.

Kwa upande wake, Devotha Kessy, ambaye alikuwa anadurufu CD, alisema kuwa alikuwa hajua kama ni kosa kudurufu CD.

Kessy alikutwa akidurufu Cd za filamu kwa mteja wake aliyejitambulisha kwa jina na Issa Salum.

Hata hivyo, Issa Salum alisema kila CD moja anayozalisha kwa Kessy huenda kuiuza kwa Sh 700.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz