Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 11 wapandishwa kortini wakituhumiwa kuwaua watu watatu

20405 Pic+mahakani TanzaniaWeb

Wed, 3 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Watu 11 wakazi wa Magange wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti mkoani Mara kwa makosa matatu ya mauaji.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo leo Oktoba 2, 2018 Ismael Ngaile mwendesha mashtaka wa Polisi, Renatus Zakeo amesema kwa pamoja wanadaiwa kuwaua watu watatu.

Amewataja washtakiwa hao ni pamoja na Mwita Mark(37) mkazi wa Magange na Romati Mwita (21) mkazi wa Arusha.

Wengine ni; Nyaisa Itelemya (35), James Nyamara (28), Godfrey Nyanda (44), Michael Machege (21), Mng'aho Chacha (34), Ghati  Makori (26), Mwita Moturi (19), Nyambega Mgaya(38) na Gikene Christopher (28) wote wakazi wa Magange.

Akisoma hati ya mashtaka katika kesi ya mauaji namba 20/2018 amesema kwa pamoja walitenda makosa Septemba 20, 2018 majira ya saa 3 usiku kijijini hapo.

Kwa pamoja waliwaua Marwa Chacha, Makori Nyamhanga na Nyangare Mahemba kinyume na kifungu namba 196 kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji, wamepelekwa mahabusu hadi Oktoba 12,2018.

Chanzo: mwananchi.co.tz