Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 11 mbaroni kujihusisha na uhalifu wa kutumia silaha za jadi

Makame Aly Ed RPC Ali Makame

Sat, 5 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu 11 wanaodaiwa kujihusha na uhalifu wa kupora simu na fedha kwa kutumia silaha za jadi nakujiita majina kama vile Damu chafu, Mazombi, Manyigu, Kaburi moja na Wafu.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo,  Ali Makame, amesema makundi ya vijana hao hufanya uhalifu huo katika kumbi za starehe, misibani na barabarani pale wanapokutana na watu hasa nyakati za usiku.

Amesema vijana hao hutumia silaha za jadi kama vile visu, nyembe, panga, bisibisi na mawe.

Kamanda Makame amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Frank Martin (21) Mathias Edwin (18) Michael Richard (15) Moses Jairo (22) Jastin Patrick (27) Cosmas Titus (17) Slvatory Zakaria (22) Abel Patrick (32) John Benito (32) Joseph Seleman (21) pamoja na Raymond Godfrey (14).

Amesema vijana hao ni wakazi mtaa wa Nsemulwa, Kazima na Majengo huku akidai upelelezi bado unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa makundi hayo na mara baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo wakabili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live