Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 11 Namtumbo wahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela

Dc Akaka Watu 11 Namtumbo wahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akiongea na waandishi  wa habari ofisini kwake Hakimu mkadhi  mfawidhi wa Wilaya ya Namtumbo  Gloria  Lwomile alisema watu 11 Wilayani Namtumbo  walihukumiwa kifungo Cha miaka 30 jela Kwa makosa ya ubakaji Kwa mwaka 2022 na mwaka 2023.

Lwomile alidai mahakama ya Namtumbo ilipokea kesi za ubakaji 17 Kwa mwaka 2022 na mwaka 2023 zilipokelewa kesi 20 na mwaka huu 2024  zimepokelewa kesi 4.

Aidha Lwomile alisema mahakama iliendesha kesi hizo ambapo Kwa mwaka 2022 kesi zilizopokelewa zilikuwa 17 na watuhumiwa waliohukumiwa na mahakama kwenda jela miaka 30 ni kesi 5 kati ya 17 zilizopokelewa .

Hata hivyo Lwomile alizitaja kesi 20 za ubakaji zilipokelewa katika mahakama hiyo  Kwa mwaka 2023 na katika hizo kesi 6 watuhumiwa walifungwa miaka 30 jela.

"Sababu ya kesi nyingi kuonekana walalamikiwa hawana hatia ni kutokana na mashauri kuondolewa mahakamani Kwa kukosa mashahidi ,Ushahidi kutokidhi vigezo vya kuthibitisha shtaka na  mashahidi kubadilika na kutotoa ushirikiano. "alisema Lwomile.

Pamoja na hukumu hizo Lwomile alifafanua kuwa  Kwa mwaka huu 2024 kesi zilizopokelewa ni 4 ambazo mahakama hiyo inaendelea kuzisikiliza .

Aliwataja waliofungwa miaka 30 jela Kwa mwaka 2022 kuwa ni Damian Mkinga (33)mkazi wa Lusewa Kwa kosa la kumfanyia vitendo vya ukatili wa kijinsia  Tabia Said(79) mkazi wa Lusewa, Juma Hassan Isilahi(19)mkazi wa Minazini Namtumbo Kwa kosa la kumtendea vitendo vya ukatili Grace Justine(10) wa Minazini, Ismail Abdallah Kayumba(26)mkazi wa Sabato Namtumbo Kwa kosa la kumtendea vitendo vya ukatili wa kijinsia  Shakila Haji Komba (14) mkazi wa Namtumbo ,Ismail Yasin Kakwela(36)mkazi wa Minazini Namtumbo Kwa kosa la kumtendea vitendo vya ukatili wa kijinsia Furaha Ismail Mfaume(5)mkazi wa Namtumbo na mwingine ni James Komba (28) mkazi wa Namabengo Kwa kumtendea vitendo vya ukatili wa kijinsia  Debora Robert Mbano(9) wa Namabengo.

Aliwataja wengine waliofungwa miaka 30 jela Kwa mwaka 2023 kuwa ni Edwin Isdory(23)mkazi wa Nahimba Kwa kumtendea kitendo Cha kikatili wa kijinsia  Merania Luambano (14) wa Nahimba ,Ramadhani Said(18)mkazi wa Namtumbo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live