Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 1000 washtakiwa kwa kuandamana Iran

Watu 1000 Washtakiwa Kwa Kuandamana Iran Watu 1000 washtakiwa kwa kuandamana Iran

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: VOA

Uongozi wa Kidini nchini Iran umejibu kutokana na maandamano ya wiki kadhaa na ukandamizaji ambao, zaidi ya kuua dazeni, pia umepelekea watu 1,000 kushtakiwa hadi sasa katika mfumo wa mahakama usio wa wazi.

Ripoti kutoka Iran zinasema waandamanaji hao kwa mara nyingine tena walipambana na vikosi vya usalama Alhamisi katika eneo lililo karibu na mji mkuu, wakiripotiwa kuwaua au kuwajeruhi wanachama wa vikosi vya usalama.

Maandamano nchini Iran yamezuka karibu kila siku tangu Septemba baada ya kifo cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wa maadili wa nchi hiyo.

Wachambuzi wanasema maandamano ya kila siku yamekuwa baadhi ya changamoto kubwa kwa Jamhuri hiyo ya Kiislamu katika historia yake.

Mapigano ya Alhamisi yalikuja baada ya maelfu ya watu kukusanyika katika mji wa Karaj, nje kidogo ya Tehran, kuadhimisha siku ya 40 tangu kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Hadis Najafi mwenye umri wa miaka 22, mmoja wa wanawake vijana kadhaa waliouawa wakati wa maandamano

Chanzo: VOA