Polisi inawasakaa watu wawili (Damien Sanderson, 31, na Myles Sanderson, 30) wanaoshukiwa kwa mauaji ya watu 10 na kujeruhi 15, wauaji hao walitumia visu kuwachoma na kujeruhi raia katika eneo Saskatchewan na kisha kutokomea kusikojulika.
Waziri Mkuu Justin Trudeau amesema tukio hilo la kuchomwa visu ni kati ya matukio 13 ya uhalifu mabaya zaidi katika historia ya uhalifu wa mauaji ya Canada na kuongeza kuwa serikali inaomboleza na kila mtu aliyeathiriwa na shambulio hilo.
Kwa mujibu wa Polisi, wanaume hao wawili walionekana wakisafiri kwa gari nyeusi aina ya Nissan Rogue na walionekana katika mji wa Regina, kilomita 320 kusini mwa kijiji cha Weldon.
Vituo vya ukaguzi vimewekwa katikati mwa mkoa wa Saskatchewan, huku wakazi wakihimizwa kujificha ndani ya nyumba na kuwa waangalifu sana wanapoendesha msako.
Ni moja wapo ya vitendo vikali zaidi vya unyanyasaji mkubwa ambavyo Canada haijapata kuona. Waziri Mkuu Justin Trudeau alitaja mashambulizi hayo kuwa “ya kutisha na ya kuvunja moyo”.
Washukiwa hao walionekana mara ya mwisho na umma huko Regina wakati wa chakula cha mchana siku ya Jumapili, na huenda walikuwa wakisafiri kwa gari nyeusi aina ya Nissan Rogue.