Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wawili wafa wakicheza kisimani

Watoto Kisimani Kifo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo

Sat, 5 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limesema kuwa limepokea taarifa ya wa watoto kufa wakati wakicheza kando ya kisima, hali ambayo ilizua taharuki katika kijiji cha Mwembetogwa mkoani Mtwara.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema, ilikuwa Machi 1 katika kitongoji cha Kiyanga kijiji cha Mwembetogwa wilayani Mtwara Vijijini watoto hao walikutwa wamefariki katika kisima.

Ametaja majina ya watoto hao ni Samia Hassan (4) na Shafiii Hamadi (3) wanaoishi na wazazi wao kijijini hapo, akisema amefariki baada ya kuzama kwenye kisima kilichokuwa na maji.

Kamanda Katembo anasema kuwa taarifa zinaeleza kuwa watoto hao waliondoka nyumbani kwao saa tano asubuhi kwenda kucheza ambapo ilipofika majira ya saa sita mchana wazazi walianza kuwatafuta kwa ajili ya chakula lakini hawakufanikiwa kuwaona.

Amesema taarifa alizopewa na wazazi wao ni kwamba, walipofika kisimani hapo walikuta nguo za watoto hao na baadaye kuona mwili wa Shafii Hamadi ukielea na kufanikiwa kuutoa huku mwili wa Samia Hassan ukizama kwenye maji.

“Miili ya watoto hao ilifanywa uchunguzi na madaktari na kubaini kuwa watoto hao wamekufa kutokana na kukosa hewa. Baada ya uchunguzi familia ilipewa kwaajili ya maziko,” alisema Katembo

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa waazazi kufatilia watoto wao wanapokwenda kucheza ili kufahamu walipo na wanacheza nani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live