Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wauawa kwa mapanga

WATOTO PWANI.webp Watoto wauawa kwa mapanga

Thu, 11 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika tukio la Pwani, mtoto mmoja aliuawa kwa kukatwa kwa mapanga kwa kilicholezwa ni wivu wa mapenzi kwa mke mkubwa kukosa mtoto wakati mke mdogo ana mtoto.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa, alisema tukio hilo lilitokea Juni 2, mwaka huu, majira ya saa 3 usiku eneo la Mji Mpya Kata ya Kisutu wilayani Bagamoyo.

Alisema mtoto huyo alikuwa na bibi yake Clemencia Mashaka (65) alipigiwa simu na namba ambayo haikufahamika, akielezwa kuwa kuna dereva pikipiki atamfuata ili ampeleke eneo la Kingani kumpa huduma mgonjwa aliyedaiwa mimba yake kuharibika.

Alisema mtu huyo alifika na kumchukua bibi na mjukuu wake na walipofika porini, dereva alisimamisha pikipiki yale na kuanza kuwakatakata na mapanga bibi na mjukuu na kusababisha kifo cha mtoto Joshua Emmanuel na majeraha kwa bibi Clemensia.

Kamanda Nyigesa aliwataja wanaoshikiliwa ni Hussein Chongo (21) dereva pikipiki mkazi wa Kimara Ng’ombe Bagamoyo, Sofia Marius (28), mkazi wa Nianjema Bagamoyo na Sofia Roman (23) wakala wa mitandao ya simu mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, chanzo cha mauaji ni wivu wa kimapenzi, kwa Sofia Marius ambaye ameolewa ndoa ya wake wawili na hajabahatika kupata mtoto, huku mwenzie akiwa na mtoto Joshua, hivyo kufanya njama za mauaji ya mtoto huyo.

Wakati huo huo, Mtoto Emmanuel John (4), mkazi wa Ndala Manispaa ya Shinyanga, anadaiwa kuuawa na mjomba wake, James Mhoja (36), kwa kuchinjwa shingoni na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.

Kaka wa marehemu, Godfrey Mhoja, alisema lilitokea juzi majira ya mchana, wakati marehemu akicheza na wenzake, ndipo alipofika mjomba wao akiwa na mapanga mawili na rungu, akamshika na kuanza kumchinja shingo.

Alisema wakati akimchinja shingo ndipo akasikia kelele ikabidi atoke nje na kumuona mdogo wake akiwa amelala chini, huku akitoka damu shingoni, na alipomzuia mjomba wao huyo alimkimbiza na yeye na mapanga.

Alisema alikimbilia ndani na baada ya hapo ilibidi aruke ukuta kisha kwenda kuomba msaada kwa majirani.

“Tulivyokuja na majirani kutoa msaada tulikuta mdogo wangu akiwa ameshachinjwa shingo na kutenganishwa na kiwiliwili, huku mjomba akianza kututishia kutukata mapanga, lakini wananchi walianza kumshambulia kwa kumpiga mawe na yeye akafariki papo hapo,”alisema Mhoja.

“Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Joseph Paulo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa chanzo cha mauaji hayo wanakichunguza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live