Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wauawa ikidaiwa ni kulipiza kisasi

Kisasipic Data Watoto wauawa ikidaiwa ni kulipiza kisasi

Fri, 4 Mar 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Watoto wawili  Ellen Jinele (5) na Diana Jinele (3) wameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na watu wasiojulikana.

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Machi 4, 2022 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda imesema kuwa tukio hilo limetokea jana Machi 3 wakati mama wa watoto hao akiwa shambani na baba akiwa machungani.

Amesema kabla ya kuuawa watoto hao waliachwa nyumbani kwa bibi yao na walikuwa na binamu wa baba yao aliyetajwa kwa jina la Sayi Ishishi aliyeishi kwenye nyumba hiyo kwa wiki moja.

“Sayi aliwachukua watoto kutoka kwa bibi yao walikokuwa wameachwa na kuwapeleka nyumbani ambako tukio lilitokea na baada ya tukio hilo alitoroka na mpaka sasa hajulikani alipo,” amesema Kamanda Chatanda.

Ameendelea kusema kuwa, miili ya watoto hao iligunduliwa na mama yao baada ya kutoka shambani alipokwenda kuvuna mahindi nakueleza kiini cha tukio hilo kuwa ni kulipiza kisasi.

Amesema inadaiwa kuwa baba wa watoto hao alikuwa akikopesha pesa kwa riba na mtu akishindwa kulipa deni alikuwa akichukua maeneo.

Advertisement Aidha mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hili.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz