Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wanusurika kutekwa, wasimulia

44745 Pic+kutekwa Watoto wanusurika kutekwa, wasimulia

Tue, 5 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Wakati wimbi la wizi wa watoto likishika kasi, watoto wawili wamenusurika baada ya kutekwa na watu wasiojulikana kuwaziba midomo na pua kisha kuwatelekeza katika jumba bovu kwa zaidi ya saa 11 katika shehia ya Kwarara, mkoa wa Mjini Magharibi.

Tukio la kutekwa kwa watoto hao Mussa Haji Khatib (14) na Khalid Haji Hassan (12), lilitokea juzi wakati wakirejea kumpeleka mwenzao shuleni.

Inaelezwa walikutana na watu wawili njiani na kukamatwa kutumia nguvu huku wakizibwa na vitambaa mdomoni.

Akisimulia mkasa huo mama mkubwa wa Khalid, Saumu Khamis Juma alisema walipata wasiwasi mkubwa baada ya kutoonekana kwa mtoto wao tangu asubuhi hadi jioni.

Saumu alieleza kuwa baada ya kufika saa 12:00 jioni walipotokea watu na kumweleza kuwa watoto wao wapo kituo cha polisi.

Akisimulia mkasa huo, Mussa Haji Khatib alisema baada ya kukamatwa na watu wasiowafahamu, waliwawekea vitambaa mdomoni na puani mithili ya pamba na kupoteza fahamu.

Alisema walikaa kwenye jumba hilo wakiwa wamefungwa toka asubuhi na walikuja kupata fahamu saa 12:00 jioni wakiwa wamefungwa miguu na mikono, hivyo walianza kupiga kelele kuomba msaada.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walisema walisikia kelele kutoka kwenye jumba hilo hivyo wakaingia kuona kilichokuwa kimewasibu watoto hao.

Sheha wa shehia hiyo Juma Kassim Chande alisema ipo haja kwa jamii kurudisha utaratibu wa malezi ya zamani kila mmoja kujali mtoto wa mwenzake kama wa kwake.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Thobias Sedeyoka alisema alipata taarifa hiyo na ataitolea ufafanuzi zaidi hapo baadaye.



Chanzo: mwananchi.co.tz