Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 5,867 wamebakwa ndani ya siku 365 Tanzania

02738cc3614ed7a65f147ee0ec0619c1 Watoto 5,867 wamebakwa ndani ya siku 365 Tanzania

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SHIRIKA la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) limesema takwimu za Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto zinaonesha kuwa wanawake 1,284 na watoto 5,867 walibakwa mwaka jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Koshuma Mtengeti alisema hayo jana Arusha wakati wa mkutano ulioshirikisha makamanda wa polisi uliozungumzia upatikanaji haki jinai kwa watoto waathirika wa ukatili wa kingono na wa kijinsia.

Mtengeti alisema ripoti hiyo pia inaonesha kuwa watoto 1,000 walilawitiwa mwaka jana wakiwemo wa kiume 885 na 115 wa kike.

Alisema kwa kipindi cha miaka mitano matukio ya ukatili wa kingono ukiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto yamekuwa yakiongezeka.

Mtengeti alisema hadi Julai 12 mwaka huu mikoa inayoongoza katika matukio hayo ni Arusha (1,697), Ilala (1,486), Tanga (1,347), Kinondoni (924) na Lindi matukio 780.

Alisema mwaka juzi yaliripotiwa matukio 6,009 ya ukatili wa kijinsia na mwaka jana yaliripotiwa matukio 7,333 hivyo kuna ongezeko la matukio 1,324.

Wakati akifungua mkutano huo jana, Kamishna wa Ushirikishwaji wa Jamii, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Dk Mussa Ally Mussa alisema changamoto kubwa inayowakabili wengi katika jeshi hilo ni kutofahamu kazi za Dawati la Jinsia na Watoto.

Dk Mussa aliagiza makamanda wa polisi wa mikoa watumie watu sahihi kwenye madawati ya jinsia na kuacha kupanga watendaji wagonjwa au wajawazito.

"Baadhi ya makamanda hamtoi uzito kwenye madawati haya na wengi mnapanga watu wasio na mafunzo ya kushughulikia masuala haya ya udhalilishaji na baadhi yenu mnapanga wagonjwa na wajawazito ambao kimsingi wakiwa hapo hawawezi sababu ya matatizo ya kiafya,” alisema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live