Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto 2365 wabakwa kwa miezi sita nchini

14840 Pic+lhrc TanzaniaWeb

Fri, 31 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jumla ya watoto 2365 wamebakwa kutoka Januari hadi Juni mwaka 2018 ambao wastani wa watoto 394 kila mwezi.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya haki za binadamu iliyotolewa  leo Agosti 30 na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Idadi hiyo imeonekana kuongezeka maradufu ikilinganishwa na nusu ya kwanza ya mwaka 2017 ambapo watoto wa kike 259 walibakwa.

Ripoti hiyo imeonyesha pia watoto 533 wamelatiwa katika kipindi hicho cha miezi sita ikilinganishwa na 12 waliolawitiwa miezi sita ya kwanza ya mwaka jana.

Akiwasilisha ripoti hiyo mtafiti wa LHRC Fundikira Wazambi amesema katika kesi nyingi ukatili huo umefanywa na ndugu wa karibu.

Amesema watoto walio katika hatari zaidi ni wenye umri kati ya miaka 3 hadi 14.

"Matukio haya ya ukatilo kwa watoto yameongezeka mara tatu ikilinganishwa na mwaka jana," amesema Wazambi

Chanzo: mwananchi.co.tz