Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watishia kutowapa Polisi ushirikiano

Ndinga Gari Polisi.jpeg Watishia kutowapa Polisi ushirikiano

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siha. Wananchi wa Kijiji cha Ngumbaru, wilayani Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, wamatishia kuacha kuwataja wauza madawa ya kulevya ikiwamo bangi wakidai kuchoshwa na tabia ya watuhumiwa kukamatwa kwa muda, kisha kurudi mtaani kuendeleza biashara hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya mtu mmoja katika Kijiji hicho (jina limehifadhiwa), baada ya kukamatwa akiuza bangi, na kwamba baada ya muda, anadaiwa amerudi mtaani huku akiendelea na biashara hiyo haramu.

Hata hivyo, akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi Digital, Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Timbuka, amekiri kulijua tukio hilo na kusema: “...mtu huyo alifikishwa mahakamani na kupewa dhamana na tunaendelea kufuatilia kama anaendelea na huo uhalifu aweze kukamatwa tena.”

Awali wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, wananchi hao wamesema jambo hilo linawavunja moyo na hasa katika jitihada zao za kupambana na dawa za kulevya

Mmoja wa wakazi hao, Julius Palanjo kutoka katika kijiji hicho, amesema Oktoba 10, mwaka huu kulikuwa na mkutano maalumu wa kijiji kuhusu hali ya ulinzi na usalama, baada ya ongezeko la vijana wadogo kuvuta bangi, huku matukio mengi ya wizi yakiripotiwa.

Amesema baada ya mkutano huo, vijana waliwataja watu wanaowauzia bangi na kwamba mmoja wa watu waliotajwa, alikamatwa polisi waliokuwa kwenye mkutano huo.

“Lakini baada ya siku mbili tulimuona amerudi na kuendelea na biashara zake, mambo haya yamekuwa yakijirudia, sasa tumeona bora tupaze sauti ili viongozi wetu wa juu wayatambue,” amesma Palanjo.

Kwa upande wake Fauzia Rashid amesema lengo la kupambana na dawa hizo za kulevya ni kuliokoa taifa na kuwanusuru vijana, hata hivyo anasema: “...lakini kama watu wanakamatwa na kuachiwa, viongozi wetu wa vijiji wanatakiwa washirikishwe ili kufahamu kwa nini wamerudi mtaani.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live