Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watendaji kata, kijiji jela kwa kuomba na kupokea rushwa

5e4d92d6f5b65dd581875d435f284313 Watendaji kata, kijiji jela kwa kuomba na kupokea rushwa

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATENDAJI wawili wa Kata na Kijiji wamehukumiwa kwenda jela ya miaka mitano au kulipa faini baada ya kupatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa,

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo jana alisema mahakama ya hakimu mkazi Dodoma imemhukumu Mtendaji wa kijiji cha Mapanga Wilaya ya Chamwino, Daus Tengeneza kulipa faini ya Sh 500,000 au kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kuridhishwa na ushahidi katika shauri la jinai namba 12/2019.

Alisema Tengeneza alikuwa akikabiliwa na mashataka ya kushawishi rushwa ya Sh 300,000 na kupokea 100,000 kutoka kwa mfugaji ili amruhusi kuingiza mifugo kijijini bila kuwa na barua ya kuhamisha mifugo.

Kibwengo alisema pia mahakama ya wilaya ya Kondoa imemhukumu mtendaji wa kata ya Thawi, Hashim Mohamed (42) katika shauri la jinai namba 26/2020, kulipa faini ya Sh 300,000 au kifungo cha miaka miwili baada ya kuridhishwa na Ushahidi kwamba alishawishi rushwa ya Sh 175,000 na kupokea Sh 80,000 ili mzazi ambaye hakumpeleka binti yake sekondari baada ya kufaulu asichukuliwe hatua.

Aidha alisema mahakama ya hakimu mkazi Dodoma imetoa uamuzi wa shauri la jina namba 145,2019 na kumhukumu Abdulhakim Kabuga (27) ambaye alikuwa BVR operetta wa Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) kulipa faini ya Sh 500,000 au kifungo cha miaka mitatu,

Awali, alifikishwa mahakamani kwa kupokea hongo ya Sh 30,000 ili amsaidie mtoa taarifa kupata kitambulisho cha uraia mapema.

Chanzo: habarileo.co.tz