Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu washikiliwa Mirerani wakidaiwa kutorosha Tanzanite

11974 Tanzanite+pic TanzaniaWeb

Mon, 23 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mirerani. Watu watatu wakazi wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamekamatwa wakidaiwa kupatikana na kilo 7.53 za madini ya Tanzanite waliyoyaficha chini ya unga uliokuwa kwenye ndoo.

Watuhumiwa walikamatwa baada ya upekuzi uliofanywa na maofisa madini, maofisa usalama wa Taifa na polisi kwenye lango la kuingia ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini hayo jana jioni Julai 22, 2018.

Akizungumzia na MCL Digital leo Julai 23, 2018 Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula amesema mwanamke anayejishughulisha na kazi ya kuchekecha mchanga na udalali wa madini anadaiwa kuhusika katika tukio hilo akiwa na wanaume wawili.

"Madini waliyaficha kwenye ndoo iliyokuwa imewekwa unga wa mahindi," amesema.

Amewataja watuhumiwa kuwa ni Judith Paulo, Midumbi Ojijo na Joshua Aguta.

Amesema thamani ya madini hayo bado haijajulikana na watuhumiwa wanashikiliwa katika kituo cha polisi Mirerani kwa mahojiano.

Soma zaidi:

Tume ya Madini yashtushwa makusanyo Mirerani kushuka

 

Chanzo: mwananchi.co.tz