Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wanaswa wizi wa mifugo

85ab4cf60209c408e22d1e67475bb57b Watatu wanaswa wizi wa mifugo

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

J ESHI la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, limewakamata watu watatu kwa tuhuma za wizi wa mifugo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni alisema watuhumiwa hao walikamatwa Tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani humo.

Hivi karibuni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki alitoa agizo kwa jeshi hilo kukamata watuhumiwa 67 wa utoroshaji wa mifugo na mazao yake.

Kamanda Hamduni alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao watatu, kunatokana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutangaza operesheni ya kudhibiti wizi na utoroshaji wa mifugo maeneo ya mipakani, hasa kutokana na taarifa kuwa kuna watu wanatorosha mifugo katika wilaya ya Ngorongoro.

Alisema upelelezi bado unaendelea kuhusu tukio hilo na utakapokamilika jalada litapelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Alitoa wito kwa wananchi kuepuka usumbufu, kwa kufuata sheria za biashara ya usafirishaji wa mifugo, kwani wasipofanya hivyo watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Ofisa Habari wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Edward Kondela alisema ripoti ya uchunguzi kuhusu utoroshaji wa mifugo mipakani, iliyowasilishwa na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Julius Mjengi kwa Waziri Ndaki ilieleza kuwa kabla ya Novemba 7, 2020, mifugo iliyokuwa inatoka kwenye minada ya awali ya Handeni na Kilindi kuelekea nchini Kenya kupitia mpaka wa Horohoro, haikuwa inafuata taratibu za forodha kama shehena nyingine.

Aliongeza kuwa takwimu za daftari la mifugo katika mpaka wa Horohoro, zinaonesha idadi ya mifugo iliyopitishwa kuelekea Kenya kwa kipindi cha miaka 17 kutoka mwaka 2003 hadi Novemba 2020 ilikuwa ni ng’ombe 24,980 na mbuzi na kondoo 9,368. Idadi hiyo ni sawa na wastani wa ng’ombe 122 na mbuzi na kondoo 46 kwa mwezi.

Chanzo: habarileo.co.tz