Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wanaswa baada ya jaribio lao kuvamia kituo cha polisi kugonga mwamba

Ed1ef84569025044 Watatu wanaswa baada ya jaribio lao kuvamia kituo cha polisi kugonga mwamba

Thu, 13 May 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

-Watatu hao walikuwa katika genge lililokuwa limevamia kituo cha polisi huko Laikipia

- Walitaka kuchukua mifugo iliyokuwa ikizuiliwa katika kituo hicho, ambayo walidai ni yao

- Ng'ombe 200 walikuwa wamepokonywa kutoka mikononi mwa wahalifu Baringo na walipaswa kukabidhiwa wamiliki wao halali

Jaribio la kikundi cha wanaume kuvamia kituo cha polisi ili kuchukua mifugo "yao" halikufanikiwa baada ya polisi kukabiliana nao na kuwashinda nguvu.

Kulingana na The Standard, genge hilo lilikuwa limevamia kituo hicho cha polisi kuwachukua mifugo hao ambao walikuwa wamepokonywa mikononi mwa majangili.

Inasemakana kuwa kikundi hicho kilianza kuwashabulia na polisi ambao walilazimika kufyatua risasi hewani kuwatawanya.

Wavamizi hao walipozidiwa nguvu na polisi walianza kutoroka mmoja baada ya mwingine kukimbilia usalama wake na kuwacha nyuma watatu kati yao waliokamatwa.

Tukio hilo lilitokea katika Kituo cha Polisi cha Kinamba katika Kaunti ya Laikipia.

Kamishna wa Kaunti ya Laikipia, Daniel Nyameti alipuzilia mbali madai ya kundi hilo akisema kuwa ng'ombe hao watakabidhiwa wamiliki wake halali ambao wlaikuwa wamekusanyika katika kituo hicho.

"Zoezi la kuwakabidhi ng'ombe hao kwa wamiliki wake halisi lilikuwa linaendelea vizuri hadi watu fulani wanaoaminika kutoka Baringo, ambako wanyama hao walipatikana walianza kuvuruga mkutano. Hatukuwa na njia nyingine ila kufyatua risasi hewani kuwafurusha," Nyameti alisema.

Ng'ombe hao 200 walipatikana wakati wa oparesheni iliyoendeshwa wili jana na maafisa wa polisi.

Ng'ombe hao walinyakuliwa kutoka kwa majambazi wa Baringo ambao walidaiwa waliiba kutoka maeneo ya Laikipia ya Wangwachi, Matuiku na Ol Moran.

Licha ya vurugu iliyosababishwa na watu hao zoezi hilo liliendelea bila wasiwasi wowote.

"Kila mtu alirudishiwaa ng'ombe wake aliyeibiwa baada ya kitambuliwa. Hatutavumilia tabia kama hiyo," Nyameti aliongeza.

Polisi sasa wako macho kukabiliana na vitendo vyovyote vya ujambazi katika maeneo hayo.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke