Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wakamatwa kwa biashara haramu ya madawa

F5027ed2095d9f39f3d6df04a10b74d7 Watatu wakamatwa kwa biashara haramu ya madawa

Thu, 28 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) inawashikilia watuhumiwa watatu kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya aina ya Heroin.

Watuhumiwa hao ni Balozi wa nyumba 50 Mtaa wa Kuwaje Kunduchi jijini Dar es Salaam, Kulwa Pazi (49) maarufu Mama Udodi, Emmanuel Maamuzi (21) na Anachati Mchongeza (20).

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za kulevya, James Kaji amesema watuhumiwa hao walikamatwa na gramu 400 na Majani makavu ya bangi kete 30.

"Maafisa wa Mamlaka walifanikiwa kukamata kiasi hicho cha dawa zikiwa zimehifadhiwa ndani ya mfuko wa nailoni," amesema Kaji.

Amesema mamlaka inaendelea kuwashikilia watuhumiwa na watafikishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Chanzo: habarileo.co.tz