Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wahukumiwa miaka 30 jela, walipora kwa kutumia silaha

LAW 660x400 Watatu wahukumiwa miaka 30 jela, walipora kwa kutumia silaha

Tue, 17 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Petro Mlongo (29), Masumbuko Sakumi (25) na Jackson Masumbuko (26) wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 baada ya kukutwa na hatia kwenye kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Walitumia panga kumjeruhi kichwani na mgongoni Zwiyo Mpemba huku wakimpora Tsh. 300,000 pamoja na simu mbili ambazo zote zina thamani Tsh. 120,000.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Geita, Sosthenes Kiiza amesema adhabu kali imetolewa kwa watatu hao kama fundisho kwa wengine wenye tabia za ukatili wa aina hiyo.

Watatu hao wameomba kupunguziwa adhabu wakisema wazazi wanawategemea lakini Hakimu Kiiza ametupilia mbali utetezi wao.

MAPYA ALIYOELEZA JAMAA ALIYEENDA KUCHUKUA FOMU KWA BAISKELI, ATAO SABABU

Chanzo: millardayo.com