Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu wahukumiwa kunyongwa, wakili apongeza upelelezi

63711 Pic+kesi

Fri, 21 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Baada ya Mahakama kuwahukumu kunyongwa hadi kufa washtakiwa watatu kwa kosa la kuua kwa kukusudia, wakili mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole amesema matukio ya mauaji ya kukata koromeo na uchomaji wa makanisa yaliyotikisa Mkoa wa Kagera vilihatarisha amani na usalama mkoani humo.

Akizungumzia hukumu iliyosomwa juzi na Jaji Lameck Mlacha katika Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, wakili huyo aliyekuwa kiongozi wa jopo upande wa Jamhuri aliwamwagia sifa wapelelezi wa matukio hayo kwa umakini wao uliofanikisha ushahidi wa kutosha na kuwafanya washtakiwa watiwe hatiani.

Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa katika kesi hiyo namba 66 ya mwaka 2017 ni Aliyu Dauda, Ngesela Joseph na Rashidi Athumani.

Washtakiwa hao wametiwa hatiani kwa mauaji ya watu wanne wakazi wa Kijiji cha Kashenge, Wilaya ya Bukoba, yaliyotokea mwaka 2017.

“Licha ya kuibua hofu, mauaji haya pia yaliibua hisia ya vitendo vya ushirikina,” alisema wakili Ngole.

Mkoa wa Kagera umewahi kukumbwa na matukio ya mauaji ya kukata watu koromeo pamoja na vitendo vya kuchoma majengo ya kanisa kabla ya vyombo vya ulinzi na usalama kuingilia kati kutafuta kiini na wahusika wa matukio hayo.

Pia Soma

Akizungumza kwa niaba ya wateja wake, wakili wa utetezi, Mathias Rweyemamu alisema wanatarajia kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

“Ni maoni yetu upande wa utetezi kuwa Mahakama haikuzingatia mateso waliyopata washtakiwa. Hata video inayowaonyesha washtakiwa walikiri kuhusika kwenye mauaji hayo inaonekana imetengenezwa,” alisema wakili Rweyemamu.

Chanzo: mwananchi.co.tz