Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu mbaroni kwa mauaji ya Flora

Pingu Law Kamanda Wilibroad Mutafungwa.

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya Frola Philimoni mfanyabiashara na mkazi wa Mtaa wa Kashishi Kata ya Nyamhongolo pamoja na hawara anayetuhumiwa kuchoma nyumba na kusababisha vifo vya watu watatu tukio lililotokea hivi karibuni.

Taarifa ya kukamatwa kwa watu hao imetolewa kwa waandishi wa habari mkoani hapa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza (SACP) Wilibroad Mutafungwa.

Alitaja waliokamatwa kupitia uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo kuwa ni Elizabeth Joseph (35) ambae ni ndugu wa marehemu mkazi wa Dar es salaam na Faida Daudi (24) fundi wa nyumba na mkazi wa Igoma jijini Mwanza wakihusishwa na mauaji ya Frola Philimoni.

SACP Mutafungwa amesema chanzo cha mauaji hayo ni migogoro ya kifamilia ya kugombania mali hivyo kusababisha mama huyo kuuawa kwa kukabwa katika maeneo ya shingo kisha kukatwa na kitu chenye ncha kali na tukio hilo lililotokea Novemba 11.

“Uchunguzi wetu umebaini kuwa Elizabeth ambaye ni ndugu wa marehemu walipanga njama na fundi huyo aliyekuwa akipaka ‘lip’ katika nyumba hiyo na kutekeleza mauaji hayo,” alisema SACP Mutafungwa

Katika hatua nyingine SACP Mutafungwa alisema jeshi hilo limemkamata Nestory John (52) mkazi wa Buhongwa jijini Mwanza hawara anayetuhumiwa kuhusika kuchoma nyumba moto na kusababisha vifo vya watu watatu (Mama na watoto wawili) lililotokea hivi karibuni.

“Baada ya msako mkali tulimkuta mtuhumiwa huyu mkoani Geita kwa Mganga wa kienyeji Samsoni Mwinamila (35) mkazi wa Sulagulwa humo akiwa anamfanyia dawa asikamatwe na polisi lakini naye tumemkamata ili ajibu tuhuma za kuficha wahalifu,” alisema SACP Mutafungwa.

John anatuhumiwa kuhusika na kuchoma Nyumba ya aliyekuwa hawara wake Eva Stephano Disemba 7 2023 katika Mtaa wa Lwanhima kata ya Buhongwa wilaya ya Nyamaga jijini Mwanza.

Moto huo ulisababisha vifo vya watu watatu akiwemo mwanamke Eva na watoto wake wawinli huku chanzo kikitajwa kuwa ni mgogoro wa mapenzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live