Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu kizimbani kwa kusafirisha kilo 1.2 ya dawa za kulevya

9d20dac40d129f37c45081f946f078ca.png Watatu kizimbani kwa kusafirisha kilo 1.2 ya dawa za kulevya

Mon, 12 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAKAZI watatu wa mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la kusafirisha kilogramu 1.2 za dawa za kulevya aina Heroin.

Washitakiwa hao, George Mwakang'ata, mkazi wa Mbagala Kuu, Andrew Paul Paul wa Kurasini na Said Mgoha Mkazi wa Mtoni Kijichi Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa shtaka lao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Rita Tarimo.

Akisoma shtaka hilo Wakili wa serikali Yusuf Aboud alidai, Juni 21, 2021 katika eneo la Kurasini Mivinjeni, wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam washitakiwa hao walikutwa wakisafirisha dawa hizo za kulevya huki wakijua ni kinyume cha sheria.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, upande wa mashitaka ulidai, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kesi hiyo iliahirishwa hadi Julai 27, 2021 kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa wote hawakutakiwa kujibu kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo na walipelekwa mahabaisi kwa sababu shtaka linalowakabili halina dhamana.

Chanzo: www.habarileo.co.tz