Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu kizimbani kwa dawa za kulevya kilogramu 91.51.

13988530c294fd366c5ed364a7fb8f42 Watatu kizimbani kwa dawa za kulevya kilogramu 91.51.

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kibaha imewapandisha kizimbani washtakiwa watatu na kuwasomea mashitaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa jumla ya kilogramu 91.51.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Upendo Mono aliyewasomea mbele ya mahakimu wawili tofauti.

Akisoma mashtaka ya Amada Tindwa na Mshamu Tindwa mbele ya Hakimu Mkazi Joyce Mushi, Mono alidai Julai 21, 2021 katika kijiji cha Tawi na eneo la Kikobo, Wilaya ya Rufiji, Mshamu alikuwa akisafirisha kilogramu 29.69 na Amada alikutwa akisafirisha kilogramu 30.04 jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Kwa upande wa Momboka ambaye alisomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Joyce Khoi, ilidaiwa Julai 21, 2021 katika kijiji cha Tawi Wilaya ya Rufiji, Pwani alikutwa akisafirisha kilogramu 31.78.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 19, 2021 itakapotajwa tena. Washtakiwa wote walikana mashtaka na walipeleka mahabusu kwa kuwa mashtaka yanayowakabili hayana dhamana kwa mujibu wa kifungu ch 29 (b) cha sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya sura ya 95 iliyorejewa mwaka 2019.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live