Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watatu Wakamatwa kwa Mauji ya Mtendaji Dar - Video

Video Archive
Tue, 12 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya mtendaji wa mtaa wa Mbezi Msumi, aliyejulikana kwa jina la Kelvin Costa Mowo (38), wakati akitekeleza majukumu yake ya kusikiliza wananchi ambao walikuwa na mgogoro wa ardhi.

Kelvin aliuawa dunia jana Jumatatu, Oktoba 11, 2021 majira ya saa 5:54 baada ya watu wasiojulikana kumvamia ofisini na kuanza kumshambulia kwa mapanga mpaka kusababisha kifo chake.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema watuhumiwa wengine bado wanasakwa ili kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Chanzo: globalpublishers.co.tz