Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania wakamatwa uhamiaji haramu Kenya

0cdbf65dc6a53d82cffb990276c79071.jpeg Watanzania wakamatwa uhamiaji haramu Kenya

Tue, 8 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAKRIBANI asilimia 65 ya wahamiaji waliowekwa kizuizini nchini Kenya wanatoka Uganda, Tanzania, Somalia na Ethiopia; Imefahamika.

Ripoti ya Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini Kenya iliyotolewa wiki iliyopita inaonyesha theluthi moja ya wahamiaji hao wanazuiliwa kwa sababu ya kuwa nchini humo bila nyaraka muhimu.

Ripoti hiyo ilisema kulikuwa na wahamiaji 530 katika magereza 55 ambayo yalitembelewa na wengi wao wakiwa wenye umri kati ya miaka 22-60.

Wakati Uganda ina wahamiaji haramu 71, Tanzania ina 43 ikifuatiwa na Ethiopia wahamiaji 23, Wasomali 20, DRC Congo 11, Rwanda 11 na Nigeria tisa.

Utafiti uliofanywa na shirika la KNCHR kwa kushirikiana na GIZ kupitia mpango wa usimamizi bora wa wahamiaji ulilenga kufikia wahamiaji 246 waliopo kwenye magereza 55.

Wahamiaji haramu hao walikamatwa kwa nyakati na maeneo tofauti na kuhojiwa katika vituo vya polisi 120, vituo 130 vya watoto na mipaka mitano ya kuingia na kutoka ikiwamo ya Namanga, Lungalunga, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi, Busia na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Kwa jumla wahojiwa 501 walishiriki katika utafiti huo katika kaunti 31 uliofanyika Oktoba. Kwa mujibu wa utafiti huo, wahamiaji waliowekwa kizuizini mara nyingi wananyimwa haki zao za kibinadamu kwani wanaishia kuwekwa pamoja na wahalifu wanaotumikia vifungo kwa kufanya uhalifu.

Ripoti hiyo ilisema inagharimu serikali ya Kenya takriban Sh bilioni 2 kila mwaka kusindikiza wahamiaji kupitia mfumo wa haki ya jinai na baadaye kuwarejesha katika nchi zao za asili. Kuanzia Machi 2019.

Chanzo: habarileo.co.tz