Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania wadakwa kusafirisha dawa za kulevya

Unga Dawa Watanzania wadakwa kusafirisha dawa za kulevya

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi ya Mapato ya Ujasusi nchini India (DRI) imewakamata Raia wawili kutokea nchini Tanzania kwa madai ya kuhusika na usafirishaji wa kilo 1.5 ya madawa ya kulevya aina ya Cocaine yenye thamani ya kati ya milioni 80 hadi 100 ya India (Tsh Bil 2.4 mpaka Bil 3) kwa kuificha ndani ya miili yao ikiwa ni tukio la saba ndani ya kipindi cha mwezi mmoja nchini humo.

Mwanzoni mwa mwezi Oktoba chombo hicho cha ujasusi DRI kilimnasa Mussa Mgonja (62) na Rashid Zamiru (23) ambao waliwasili kutoka Addis Ababa nchini Ethiopia kuelekea jijini Mumbai nchini India.

Ingawa utafutaji wao wa binafsi haukuzaa Matokeo, Kwa mijibu wa ripoti, walipopelekwa katika Hospitali ya JJ, Musa alionekana na vidonge 79 ndani ya mwili wake na Rashid akiwa na vidonge 33 kisha uchunguzi zaidi ulibaini kuwa wawili hao walikuwa wabebaji mahiri wa dawa za kulevya ambapo Mussa alisema hiyo ilikuwa ni safari yake ya pili na alikuwa amesafirisha vidonge kufikia 125 vya madawa huko kuelekea jijini Delhi, nchini India.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live