Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania 1200 wadakwa kwa dawa za kulevya

Watanzania 1200 Wadakwa Kwa Dawa Za Kulevya Watanzania 1200 wadakwa kwa dawa za kulevya

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema Watanzania 1200 wamekamatwa katika nchi mbalimbali wakituhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Aidha, imesema hakuna takwimu rasmi za Watanzania ambao wamenyongwa kwasababu ya kukamatwa na dawa za kulevya huku ikitumia nafasi hiyo kueleza kwamba nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania zinatumika kama mapito ya dawa za kulevya.

Akizungumza mbele ya wahariri wa vyombo vya habari wakati wa semina iliyoandaliwa na DCEA yenye lengo la kuwajengea uelewa Wahariri na kuelezea majukumu yake, Kamishina wa Kinga na Tiba wa mamlaka hiyo Dk. Peter Mfisi amefafanua kumewepo na taarifa za Watanzania kukamatwa nchi mbalimbali wakituhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya.

"Mamlaka tunachoweza kueleza hatuna takwimu za idadi ya Watanzania ambao wamenyongwa kwa sababu ya kukamatwa na dawa za kulevya nje ya Tanzania. Tunazo takwimu zinazonesha watanzania 1200 wamekamatwa kwa dawa za kulevya nje ya Tanzania,"amesema Dk.Mfisi.

Amefafanua kwamba baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya na Somalia zimekuwa zikitimika kama mapito ya kupitisha dawa za kulevya.

Kuhusu swali la wapi watuhumiwa wa dawa za kulevya wanakamatwa kati ya Tanzania na nchi nyingine ambapo amejibu kwamba kwa Tanzania watu wengi wanakamatwa kwa dawa mbalimbali za kulevya akitoa mfano kwamba watu 800 wamekamatwa nchini katika kipindi kifupi.

Kuhusu kuteketekeza dawa za kulevya kama Bangi, Heroine na Cocaine amesema uteketezaji wa dawa hizo uko kwa mujibu wa sheria ambayo inaeleza jinsi ya kuziteketeza huku akitumia nafasi hiyo kueleza umuhimu wa waandishi wa habari kushirikiana na Mamlaka hiyo kuendelea kushirikiana kutoa elimu kwa umma ili kukomesha dawa za kulevya.

Hata hivyo Mamlaka hiyo imeeleza mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni la kila mmoja wetu huku ikiendelea kuwaomba wahariri na waandishi wa habari wasiripoti taarifa zinazohamasisha matumizi ya dawa za kulevya kwani madhara yake ni makubwa katika jamii ya Watanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live