Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano mbaroni wizi wa mifuko 128 ya mbolea

1b61802db0fd2782a364c5412b70f5c9 Watano mbaroni wizi wa mifuko 128 ya mbolea

Sat, 24 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

POLISI mkoani Tabora linawashikilia watu watano kwa tuhuma ya wizi wa mifuko 128 ya mbolea aina tofauti inayodaiwa kuwa ni mali ya Chama Kikuu cha Ushirika wa zao la Tumbaku cha Mirambo Co-operative Union cha wilayani Urambo, mkoani hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa alisema mifuko hiyo ya mbolea ilikuwa kwa ajili ya kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara katika msimu ujao wa kilimo wilayani humo.

Mwakalukwa alisema wizi huo ulifanyika Oktoba 12 mwaka huu saa 12 jioni katika mtaa wa Kitega Uchumi, Kata ya Urambo.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, watuhumiwa waliokamatwa ni Samson Nestory (35) akiwa na wenzake wanne kwa kosa la wizi wa mbolea hiyo ambayo inadhaniwa kuwa ni mali ya chama hicho kikuu cha wakulima wa Tumbaku wilayani urambo

Mwakalukwa alisema kwamba baada ya uchunguzi wakina ilibaininka kwamba watuhumiwa hao walitoa ushirikiano na kufanikiwa kukamatwa kwa mifuko 95 ya mbolea aina ya NPK.

Alisema baada ya kufanya msako huo katika ghala la kuhifadhi vitu la Jackson Musa (45) maarufu kama Mponeja, Polisi walikamata mifuko 33 ya mbolea ikiwa imehifadhiwa kwenye ghala la pembejeo.

Kamanda alisema kwamba kukamatwa na watu hao nikufuatia mwendelezo wa jeshi la polisi mkoani hapa kufanya msako ya kila siku dhidi ya wahalifu sehemu mbalimbali za mkoa huo.

Chanzo: habarileo.co.tz