Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano mbaroni tuhuma za mauaji

D2D27086 9E49 4382 87A8 C0C1BB29DC7A.jpeg Watano mbaroni tuhuma za mauaji

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

< Watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Mange Washa mwenye umri wa miaka 49 ambae inadaiwa aliuawa kwa kukatwa na panga na kichwa chake kutenganishwa na kiwiliwili wakimtuhumu kumfukuza mtoto wake nyumbani

Miongoni mwa wanaoshikiliwa ni Hoka Mazuri  ambaye ni mke wa mwanaume pamoja na watoto wake   Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema tukio limetokea tarehe 1 ya mwezi huu katika Kijiji cha Kiliwi kata ya Bupamwa wilayani Kwimba mkoani humo ambapo inadaiwa mwanaume huyo alikuwa na ugomvi na familia yake uliodumu kwa muda mrefu

Inadaiwa mtoto wake mmoja alikuwa anatuhumiwa kwa wizi ndipo akamfukuza na kupelekea mama yake ambae ni mke wa marehemu kukasirika na kupanga pamoja na Watoto wake wawili kumuua mume wake huyo na  kuwakodisha watu wengine wawili aliowalipa shilingi laki nane

‘Uchunguzi wa awali umebaini kuwa Hoka Mazuri mwenye miaka 48 mke wa Mange Washa hakuwa ameridhia kitendo cha mumewe kumfukuza pale nyumbani kijana wao aitwaye Masunga Mange miaka 28 hivyo alipanga na baadhi ya Watoto wake ili wamuue mume wake na akishafariki Masunga ataenda kuishi nyumbani hapo bila usumbufu wowote na waliwatafuta watu wengine wawili wakawalipa shilingi laki nane ili wamuuwe mwanaume huyo’

Kamanda Mutafungwa amesema upelelezi utakapokamilika watuhumiwa hao watano watafikishwa mahakamani,

Katika tukio lingine Jeshi la polisi Mwanza linamshikilia mwanamke mmoja aitwaye Marry Seni mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa jiwe kuu, Kitangiri kwa tuhuma za kutupa kichanga cha miezi saba chenye jinsia ya kike

‘Baada ya mahojiano ya kina yakiambatana na uchunguzi wa kidaktari imethibitika kuwa ndiye aliyehusika na kutupa mtoto huyo mchanga kwa kile anachodai ni ugumu wa Maisha kwa aliyempatia ujauzito huo amemtelekeza upelelezi ukikamilika tuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani’

Aidha kamanda Mutafungwa amesema watuhumiwa 104 wamekamatwa kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa tuhuma za makosa mbalimbali yakiwemo ya wizi wa televisheni, radio, kujihusisha na bangi, na Mirungi  na kwamba oparesheni hiyo ni endelevu na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live