Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano mbaroni mauaji ya mwalimu

4dffba7445b663931875f7a0b45414a5.jpeg Wahalifu walichukua TV, Subwoofer na Pasi

Tue, 3 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewakamata watu watano kwa tuhuma za mauaji ya mwalimu wa Shule ya Sekondari wasichana Bwiru, Ambrose Mapembegashi.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Ramadhan Ng’anzi, alisema mwalimu Mapembegashi aliuawa Aprili 29 mwaka huu saa 4 usiku katika makazi yake kwenye shule hiyo Kata ya Pasiansi.

“Wahalifu waliingia katika nyumba ya marehemu na kutekeleza mauaji hayo pamoja na kuchukua TV ya Itel model A243LAE, subwoofer aina ya sea piano model SP 661 pasi aina ya Africab model JT-22512,” alisema Kamanda Nga’nzi.

Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, watuhumiwa waliokamatwa ni Justine Lucas na Daniel Edward ambao ni wakazi wa Kata ya Bwiru, Paschal Nyamhanga mkazi wa Kata ya Kitangiri, Hussein Swalehe mkazi wa jiwe kuu na Elias Jonas mkazi wa Bwiru Press. Kamanda Nga’nzi alisema watuhumiwa walishikwa na mali hizo katika maeneo ya Kitangiri, Nyasaka na Bwiru.

Alisema upelelezi unakamilishwa na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani. Katika tukio lingine, polisi inawashikilia wahamiaji haramu 68 raia wa Ethiopia kwa kosa la kuingia nchini bila kibali. Kamanda Nga’nzi alisema wahamiaji hao walikamatwa Aprili 29 saa 11:30 jioni katika Kijiji cha Sanjo, Kata ya Usagara wilayani Misungwi na akasema wana umri wa kati ya miaka 14 hadi 25.

Alisema wahamiaji hao walikuwa wamehifadhiwa na mwanamke anayeitwa Tarica Alex ambaye pia naye alikamatwa kwenye nyumba ya mtu anayefahamika kwa jina moja la Joseph.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live