Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watano kizimbani kwa kuingiza kemikali Tanzania

43929 Watanopic Watano kizimbani kwa kuingiza kemikali Tanzania

Tue, 26 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watu watano wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka manne ya kuingiza kemikali nchini bila kuwa na vibali.

Washtakiwa hao, Jumanne Mazunde, Godfrey Kiwelu, Nsia Mbonika, Chankan Mhina na Joseph Omollo wamesomewa mashtaka leo Jumanne Februari 26,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Huruma Shahidi.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amedai kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa manne ya kuingiza nchini kemikali mbalimbali zikitokea Nairobi, Kenya.

Katika shtaka la kwanza linalomkabili Mazunde, anadaiwa  Septemba 13, 2017  aliingiza nchini kemikali aina ya Potassium Hydrochloride kilo 12.5, Amonium Chloride 99%.

Kosa la pili linamkabili Mbonika na Mhina wanaodaiwa  Septemba 13, 2017 kuingiza kemikali aina ya Potassium Hydrochloride kilo 7.5 na Sodium Hydrogen Carbonate kilo 29.

Kosa la tatu linamkabili Mhina anayedaiwa Septemba13, 2017 kuingiza kemikali aina ya Polyester resin kilo 100.

Katika shitaka la nne  linalomkabili,  Omollo  anadaiwa  Septemba 13, 2017 aliingiza kemikali hizo.

Baada ya maelezo hayo, wakili Wankyo  amedai upelelezi wa shauri hilo umekamilika na  kuomba terehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa hao walikana mashtaka yanayowakabili huku Hakimu Shahidi akieleza kuwa dhamana yao ipo wazi.

Washtakiwa Kiwelu, Mbonika na Mhina walitimiza masharti ya dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 12, 2019 itakapotajwa tena.



Chanzo: mwananchi.co.tz